Updates

Duru Za Kitaifa

Sherehe za Idd zafana Dar, mikoani

Kufuatia kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislamu nchini wametakiwa kudumisha ukarimu, mapenzi, huruma san- jari na kuendelea na utekelezaji wa ibada walizokuwa wakizifanya ndani ya mwezi huo kwa kuzifanya ndani ya miezi mingine isiyokuwa Ramadhani. Hayo yamebainishwa na masheikh mbalimbali walipokuwa wakiwahutubia mamia ya wau- mini wa dini ya Kiislamu kupitia khutba ya ibada ya Swala ya ...

Read More »

Saruji ya Dangote kujenga Makao Makuu Dodoma

Na Jasmine Shamwepu TAASISI ya Dangote inayojishughulisha na uzalishaji wa saruji kupitia kiwanda chake kilichopo mkoani Mtwara imesema itafungua kituo kikubwa cha uuzaji wa saruji mkoani Dodoma. Mbali na hilo, kampuni hiyo ina mpango wa kujenga bandari kavu ambayo itatoa huduma katika mikoa na nchi jirani kwa lengo la kuwarahisishia upatikanaji wa saruji ya uhakika. Makamu wa Rais wa kampuni ...

Read More »

Jamii ya Wasomali Tanzania Yachangia Baa la Njaa Somalia

NA MWANDISHI WETU Jumuiya ya Wasomali waishio nchini wamefanikiwa kuchanga jumla ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zao wa Somalia wanaokabiliwa na baa la njaa nchini Somalia. Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Sheikh Abdulqadir Mohamed Al-Ahdal amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuchangisha shilingi milioni 50 huku lengo likiwa ni kupata shilingi za Kitanzania ...

Read More »

TAHAFE Kutoa Tamko la Hijja

na mwandishi wetu Shirikisho la Mahujaji hapa nchini (TAHAFE) limesema kuwa ndani ya wiki moja ijayo litatoa tamko juu ya sakata la HijJa ili kuondoa taharuki iliyopo. Katika mazugumzo kwa kupitia simu, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Sheikh Abdallah Khalid aliahidi kutoa tamko hilo kufuatia habari iliyochapwa toleo la wiki iliyopita la gazeti hili kuhusu lawama zinazoelekezwa kwenye shirikisho hilo ...

Read More »

Watanzania Waonesha Matumaini Kwa Taasisi ya Kikwete

NA ABDULKARIM MSENGAKAMBA. Baadhi ya Watanzania wameonesha kuwa na matumaini makubwa kwa taasisi mpya ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (JMKF) katika kusaidia kutatua changamoto mbali mbali hapa nchini na katika Bara la Afrika. Wakazi hao waliohojiwa walisema Kikwete ni mwanadiplomasia anayekubalika kimataifa na hivyo atakuwa na uwezo mkubwa wa kuvutia rasilimali fedha kutoka kwa wafadhili katika taasisi yake. Pia walisema ...

Read More »