Updates

Jamii ya Wasomali Tanzania Yachangia Baa la Njaa Somalia

NA MWANDISHI WETU

Jumuiya ya Wasomali waishio nchini wamefanikiwa kuchanga jumla ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zao wa Somalia wanaokabiliwa na baa la njaa nchini Somalia. Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Sheikh Abdulqadir Mohamed Al-Ahdal amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kuchangisha shilingi milioni 50 huku lengo likiwa ni kupata shilingi za Kitanzania milioni 300. “Tumefanikiwa kuchangia milioni 50 mpaka sasa lakini tunahitaji shilingi milioni 300 ili kuwaepusha ndugu zetu wa Somalia na baa la njaa,” alisema Sheikh Al-Ahdal. Sheikh Al-Ahdal pia alitoa wito kwa watu mbali mbali juhudi hizo ambazo zitawaokoa wanawake na watoto wa Somalia wanaokabiliwa na tishio hilo kubwa la njaa. Tayari Umoja wa Mataifa (UN) umeshatangaza kuwa watu Milioni 6.2 nchini Somalia wanakabiliwa na njaa kali kutokana na ukame ulioikumba nchi hiyo. Nalo Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limeonya kuwa imesalia miezi mwili tu ili kuepeuka hali hiyo iliyowahi kulikumba taifa hilo mara tatu ndani ya miaka 25 iliyopita ambapo njaa ya mwisho ya mwaka 2011 iliu w a w a t u t a k r i b a n i 260,000. Pia imetajwa kuwa watoto takribani 363,000 wanakabiliwa vikali na utapiamlo na wanahitaji msaada wa haraka wa chakula. Takribani wiki moja iliopita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres aliwasili kwa dharura nchini Somalia ikiwa ni jitihada za kushawishi dunia itoe msaada kwa taifa hilo. Guterres alisema dunia inapaswa kuchukua hatua za haraka sana. Nayo Serikali ya Somalia chini ya Rais mpya Mohamed Abdullahi Mohamed (Farmajo) ilitangaza hali hiyo ya ukame na tishio la njaa kuwa ni janga la kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*