Updates

Nafasi na Utakatifu wa Nyumba za Ibada katika Uislamu na Uharamu wa Kuzishambulia

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Peke Yake, na rehema na amani zimfikie Yule ambaye hakuna Nabii baada yake. Ama baada ya hayo, Dini ya Kiislamu inahimiza kuzilinda na kuzihifadhi nyumba za iba- da kwenye mataifa ya Kiisla- mu kwani suala la usalama na kulinda watu kwenye jamii ya Kiislamu ni moja ya misingi ya sharia ya Kiislamu. Kwa wasio Waislamu na ambao wanaishi na Waislamu katika jamii ya Waislamu wali- dhihirikiwa na uzuri wa dini kwa kuishi pamoja na kwa ku- vumiliana nasi. Hii ni kwa sababu kulikuwa na kitu kili- chokuwa kinalinda uhuru wao wa kuabudu. Aidha, hali hiyo ya kuvumil- iana huwafanya wananchi wawe pamoja na washirikiane kwa uhuru, heshima, kutoten- gana wala kubaguana. Kwa mfano, Allah ameka- taza kujadiliana na wasio Waislamu na hasa hasa watu wa Kitabu, na kama hakuna budi kujadiliana basi majadi- laiano yawe kwa njia nzuri zai- di. Allah anasema: “Wala msi- jadiliane na watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni, ‘Tumeyaamini yaliyoterem- shwa kwetu na yaliyoterem- shwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake’” (Qur’an, 29:46]). Uislamu ni dini ya mtu bin- afsi na jamii kwa ujumla. Paia Uislamu unahimiza kuwa na jamii huru inayoishi kidugu, kutegemeana, kuvumiliana na kumfanya kila mmoja ajihisi kuwa ana jukumu la kuijenga na kuilinda amani. Dini Tukufu ya Kiislamu imechukua dhamana ya kulin- da uhuru wa ibada kwa wasio Waislamu na kuheshimu ima- ni zao, ibada zao, sikukuu zao sherehe zao, maadhimisho yao, mapumziko yao, na ku- ruhusu uanzishwaji wa ma- jengo yao ya ibada, na kuhak- ikisha wanayalinda, wanay- akarabati na kuheshimu mila na desturi zao. Na ikifikia hatua mmoja wa washirikina anapomuomba Muislamu ulinzi, hana budi Muislamu kutekeleza ili kum- uepusha na madhara hadi afike kwenye sehemu yake salama, ambako ni nyumbani au kwenye makao yake. Allah anasema: “Na ikiwa mmoja wapo katika washiriki- na akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa ama- ni. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu,” (Qur’an, 9:6).Na huko kuvumiliana, hufi- kia kilele cha mazoezi na ku- tenda kwenye kijamii kwa ku- fuata maelekezo ya Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) pale aliposema: “Mtu mwenye kumuudhi aliye dhamanani, atakuwa hasimu wangu, na atakayekuwa hasimu wangu, nitahasimiana naye Siku ya Kiyama”. Na haya ni maelekezo yaliyotekelezwa na Makhalifa waongofu. Na sheria za Uislamu zime- wapa wasio Waislamu waishio kwenye jamii ya Kiislamu hi- fadhi na ulinzi wa mali zake, heshima zake. Na ulinzi huu ni endelevu kwa watu wa dini nyingine au wananchi wanaoi- shi kwa dhamana maalumu muda wa kuwa wanatii maku- baliano. Hivyo, suala la kuwa- hakikishia ulinzi wasio Wais- lamu ni dhamana ya kisheria kwani viwiliwili na nafsi vina- hitaji kulindwa kwa mujibu wa makubaliano ya Waislamu na viongozi wakombozi wa Ki- islamu kwenye mikataba na makubaliano yote waliyoing- ia. Sheria za Kiislamu zilizot- eremshwa kutoka kwa Allah zimebainisha na Mtume (re- hema na amani ya Allah iwe juu yake) amelekeza kuwahak- ikishia usalama wa nafsi na mali wasio Waislamu wanaoi- shi kwenye jamii wa Waisla- mu, muda wa kuwa wanatii yaliyo kwenye sheria. Sheria za Kiislamu zipo wazi, na hazikuwekwa kama mbadala wa kimaslahi kati ya Waislamu na wasio waislamu, na wala hazikuwekwa na she- ria za kimataifa au mataifa ya Kiislamu nk; bali hukumu hizi ni muhimu katika sheria ya Kiislamu ambazo nchi inatak-iwa kuzitumia na kuzitekeleza. Hakika huu ni wajibu kwa kidini kabla hayajakuwa maslahi ya kisiasa au kufuata sheria za kimataifa. Uislamu unaanzisha jamii safi ya kiutu na unaimarisha uhusiano kati ya watu wote juu ya misingi madhubuti ya wema na kuoneana huruma. Uislamu haukuacha uhusiano na wasio Waislamu kwa saba- bu ya tofauti za utashi au maslahi, mielekeo ya kikabila, rangi au chuki ya kidini. Na sheria zilizowekwa na Uislamu zinasifika kwa kui- marisha uhusiano na Waisla- mu na wasio Waislamu, uvu- milivu, kurahisisha mambo, kuhifadhi haki na kuepuka uonevu. Allah anasema: “Na hakika tumewatukuza wanadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tume- waruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba,” (Qur’an, 17:70). Na Mtume (rehema na am- ani ya Allah zimshukie) amesema: “Mtu anayemuua aliye kwenye dhamana hatonusa harufu ya pepo, na harufu ya pepo inasikika um- bali wa miaka arobaini”. Ima- mu Maliki na Al Laithi wa- nasema: “Muislamu ataka- pomuua mtu anayeishi kwa amani naye huuliwa”. Na Imamu Sha’abiy na Abuu Hanifa kuhusu suala la Muislamu kumuua asiye Muislamu wamesema kwa ujumla wa andiko la kudumu linalowajibisha kisasi, ni kuwa suala la kulinda damu linawa- husu wote. Mtume (rehema na amani ya Allah zimshukie) amebaini- sha uharamu wa kuwasham- bulia watu wa dini, Wayahudi na Wakristo pale aliposema: “Mtawakuta watu wanaodai wameziweka wakfu nafsi zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi waacheni na madai yao.” Na kanuni ya dhahabu ya Maimamu wa fiqh inaeleza kuwa kasisi na mtawa wapo huru, hawauawi wala hawakamatwi mateka na hu- takiwa waachwe huru kwa ka- diri iwezekanavyo kulingana na nyenzo za kimaisha. Aidha, Sharia ya Kiislamu inaharamisha kuharibu ny- umba za ibada zisizo za Wais- lamu zilizo kwenye nchi ya Ki- islamu, hata zikiwa kwenye miji ya kale, na wala hakuna shaka Swahaba na Matabiyna (Allah awaridhie) walipoikom- boa miji walizitambua katika hali ya vita na amani na waka- ziacha. Na kwenye hili Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Na lau kuwa Mwenyezi Mun- gu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingelivun- jwa nyumba za watawa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu lina- tajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu hum- saidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu,” (Qur’an, 22:41).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*