Updates

Qur’an Inasemaje Ndugu Wanapogombana?

Mapema wiki hii, baadhi ya nchi zinazounda Umoja wa Ghuba (GCC) zilisitisha uhusiano wao wa Kidiplomasia na nchi ya Qatar. Nchi hizo ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Bahrain, Yemen, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Kisi- wa cha Maldives. Kuna mengi yametajwa kama chanzo cha mvutano huo, lakini sisi kama chombo cha habari cha Kiislamu kinachopendelea na kuhimiza maelewano baina ya Waislamu, hatutaki kujadili sababu, kiiini cha tatizo na ku- laumu upande wowote. Badala yake, sisi tunapendelea zaidi kutazama athari za hali hiyo na nini kifanyike katika kureje- sha umoja. Mara tu baada ya uamuzi wa tangazo la kusitisha uhusiano na Qatar lililotolewa na mataifa tu- liyoyataja, nchi hiyo ndogo katika eneo la Mashariki ya Kati lime- athirika kwa namna nyingi kati- ka nyanja mbalimbali za bi- ashara, mawasiliano na chakula Kwanza, usafiri wa anga ni miongoni mwa sekta za kiuchu- mi zinazotegemewa mno na Qa- tar kutokana na Shirika lake la ndege (Qatar Airways) kufanya safari nyingi katika miji mbalim- bali ndani na nje ya nchi za Ghu- ba ikiwemo Dubai, Abu Dhabi, Riyadh na Cairo, na tayari nchi hizo zimepiga marufuku Qatar kuingiza ndege zake katika nchi hizo.Wachambuzi wanaamini kuwa, hali hii huenda ikaiathiri Qatar kimapato. Katika sekta ya ujenzi, kwa sasa Qatar inaendelea na ujenzi wa bandari, ukanda wa kitabibu na miradi mingine ya maendeleo ambayo hata hivyo vifaa vingi vya ujenzi wake huagizwa kutoka Saudi Arabia. Hivyo basi, kufun- gwa kwa mpaka baina ya Saudi Arabia na Qatar, huenda ku- kaathiri ujenzi huo. Pia, kuna suala la chakula am- bapo Qatar inategemea kwa kiasi kikubwa chakula kutoka nje ya nchi na inatajwa kuwa asilimia 40 ya vyakula inapitia katika mpaka huo uliofungwa. Hali hiyo inatajwa huenda ikaiathiri Qatar. Ukiacha athari kwa upande wa Qatar, tutakuwa tunajidan- ganya tukisema nchi hizo zili- zokata uhusiano na jirani yao nazo hazitaathirika kwa sababu ukweli ni kwamba Qatar ime- kuwa ikifanya biashara na karibu nchi zote hizo ambazo iko katika mgogoro nazo. Na ukiangalia sana, wananchi wa nchi hizi ni ndugu siyo tu kwa Uarabu wao, lakini muhimu zaidi ni undugu katika Kiislamu. Hakuna undu- gu mkubwa kama huu. Kwa sababu hiyo basi, Gazeti la Imaan linatoa rai kwa viongozi wa nchi hizi kujadili tofauti zao na kuzi- maliza ili kurejesha uhusiano wao mzuri kama zamani. Ni kawaida kwa wanadamu wanapoishi pamoja, kutokana na udhaifu wa kibinadamu kugom- bana na hii ni fitna na mtihani kwetu. Kwa mujibu wa Quran na Sunna, inapotokea Waislamu wametofautiana na kuhasimiana kama hivi au zaidi ya hivi yat- akikana pande mbili zinazogom- bana kufanya mazungumzo ya amani ili kupata suluhu ya kudu- mu na yenye maslahi kwa pande zote. Allah anasema: “Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhu- lumu mwenzie, basi lipigeni li- nalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mun- gu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki,” (Qur’an, 49:9). Kwa kauli hii ya Mwenyezi Mungu, tunasisitiza tena umuhimu wa mapatano baina ya mataifa haya kwani sote ni umma mmoja wa Kiislmu. Muhimu zaidi, wakati viongozi wa mataifa haya waki- tafuta maelewano wakumbuke kuwa Waislamu wengi duniani wanategemea uongozi wao kwa namna moja au nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*