Updates

ramadhani ituandae kutekeleza ibada ipasavyo

Hakika Mwenyezi Mungu amewaumba majini na wanadamu kwa hekima na lengo maalum, nalo ni kumuabudu Yeye Peke Yake. Pamoja na ukweli huo wan- adamu wengi wanaamini kuwepo kwao duniani ni kwa bahati tu (by chance).

Pia, kuna waliochupa mipaka na kudha- ni kuwa uhai wa duniani hauna lengo jin- gine lolote zaidi ya kustarehe na kusubiri kifo. Miongoni mwa hao ni mwanafalsafa Karl Max ambaye anasema: “Kuwepo kwa binadamu hapa duniani ni kwa ajili ya ku- timiza matakwa ya kinyama, yaani kula, ku- zaliana, kulala, kutimiza matakwa ya kimwili na kusubiri kifo, na baada ya hapo hakuna la ziada.” Yaani hakuna pepo, moto, ufufuo wala Kiyama.”

Hii ni dhana batili ambayo Muislamu hapaswi kuiamini, kama Allah Aliyetukuka anavyobainisha katika Aya ifuatayo: “Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo- mo ndani yake bure. Hii ni dhana ya wale waliokufuru. Basi adhabu kali ya moto ita- wathibitikia wale waliokufuru,” (Qur’an 38:27). Allah Aliyetukuka akasema katika Aya tena: “Je, mlidhani ya kwamba tumeku- umbeni bure (bila sababu) na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?”(Qur’an, 23:115).

Kwa muktadha huo, ni wazi lengo kuu la kuumbwa kwetu ni kumuabudu Allah, yaa- ni kutii amri zake wakati wa shida na raha. Hiyo ndiyo ibada na Uislamu. Hivyo, yeyote atakayefanya jeuri na kiburi cha kutokufan- ya ibada atakuwa ni mwenye kupuuza heki- ma ambayo viumbe wameumbwa kwa sababu hiyo.

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka anatufa- hamisha: “Sikuwaumba majini na wanada- mu ila wapate kuniabudu,” (Qur’an, 51:56).

Ramadhani ni mwezi ambao Waislamu wengi hujitahidi kutekeleza ibada mbalim- bali za faradhi na Sunna. Hii ni kwa sababu, katika kivuli cha usafi na utakasifu utokanao na swaumu, mfungaji hajizuii tu kula na

kunywa katika wakati ulioainishwa, bali pia huzuia viungo kama macho, miguu na ulimi kufanya mambo yaliyoharamishwa.

Kwa maana nyingine, kufaradhishwa swaumu kwa wanadamu wa kila zama ni kwa ajili ya faida na maslahi yao ya hapa duniani na kesho akhera. Hivyo, ili kufikia lengo tunapaswa kudiriki sababu ya kuwe- po swaumu na kuitekeleza kwa kufuata ma- fundisho sahihi ya dini.

Kwa namna hii, tutaweza kufikia daraja ya juu ya UchaMungu na hivyo kufikia kilele cha ibada.

Kama inavyofahamika, mafundisho ya Uislamu ni mjumuiko wa sheria muhimu katika uhai wa mwanadamu ambazo hum- fanya mja kutekeleza wajibu wa kuabudu ipasavyo.

Mwenyezi Mungu amewapendelea Waumini Mwezi wa Ramadhani ili uwe daraja la kufikia lengo la kuumbwa kwao,

na kwa ajili hiyo Waislamu hufanya hima ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na ibada za funga, swala, zaka, kusoma Qur’an, kumdhukuru Allah, kusaidia masi- kini na nyinginezo kupitia darasa za misikitini na katika vipindi maalum vya ra- dio na televisheni.

Hata hivyo inashangaza kuona Waisla- mu wengi hawahudhurii darasa za mafunzo ya dini hata wanapokumbushwa kufanya hivyo. Badala yake wanapoteza muda mwingi katika vibaraza vya mazugumzo yasiyofaa na kushiriki michezo ya pumbao ikiwemo karata, drafti, kete, bao, dhumna, kusikiliza nyimbo na kupiga manyanga na ngoma za kula daku wakati wa usiku.

Michezo yote hii ni haramu; haifai, kwa sababu inapumbaza akili na kumfanya Muislamu asahau kushughulika na mambo muhimu ya kiibada.

Ni dhahiri kuwa, darasa za Ramadhani zina nafasi kubwa katika kuathiri moyo wa mja katika kuiendea ibada. Hivyo kila Muis- lamu aweke nia na azma ya kuisoma dini na kutekeleza ibada mbalimbali za faradhi na sunna ili itakapomalizika Ramadhani iwe rahisi kudumu nazo.

Sanjari na hivyo tunawajibika kujifunza kusoma Qur’an kwa usahihi na mazingatio katika mwezi huu ambao ndani yake ime- teremshwa Qur’an.

Na katika kuonesha ubora na umuhimu wa kusoma Qur’an, Malaika Jibril alikuwa akishuka ndani ya mwezi huu kwa ajili ya kumsomesha Qur’an Mtume (amani na re- hema ya Allah zimshukie).

Kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud (Allah amridhie), Mtume (rehema na amani ya Al- lah imshukie) amesema: “Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah atapata jema moja, na kila jema moja ni sawa na thawabu kumi, wala sisemi ‘Alif-laam-mi- ym’ ni herufi moja, bali ‘Alif ’ ni herufi moja na ‘lam’ ni herufi moja na ‘miym’ ni herufi moja” (Tirmidhiy).

Juu ya hayo, tunawajibika kumuabudu Allah kikamilifu, na si kuchagua baadhi ya ibada na kuacha nyinginezo. Katika kulion- ya hilo Allah anatuambia: “Enyi mlio- aamini! mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife isipokuwa mmekwisha kuwa Waislamu”(Qur’an 3:102).

Tunamuomba Allah atuwafikishe katika kufanya mambo ya kheri ndani ya Ramad- hani, pia atuwezeshe kufuata mafundisho ya Mtume Muhammad (rehema na amani ya Allah imshukie) katika maisha yetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*