Updates

Last Sober House: Kituweo cha Mbuzi

UONGOZI wa kituo cha kuwahudumia vijana walioathirika na dawa za kulevya, cha Free at Last Sober House, cha kihonda Mjini Morogoro, umeishukuru Taasisi ya The Islamic Foundation kwa kuwapatia kituweo cha Mbuzi.

Uongozi wa Kituo hicho umetoa shukurani hizo, ikiwa imepita siku moja baada ya Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation kuwaahidi kuwapa Mbuzi, kwa ajili ya kituo kwa Vijana wanaohudumiwa katika Kituo hicho.

Mkurugenzi wa Kituo cha kuwahudumia Walioathirika na Dawa hizo, Juned Mbarak ameishukuru Taasisi ya The Islamic Foundation kwa kuonyesha nia ya kuwa pamoja na Vijana hao kwa kuwasaidia misaada mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*