Updates

TIF Kumleta Nchini Mhadhiri Wahaj Tarin

 

Mwenyekiti wa TIF, Arif Nahdi, akiwa na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Al Ka’abi, ofisini kwa Mufti huyo mjini Unguja. Katika mazungumzo yao Mufti na Mwenyekiti walikubaliana kushirikiana karibu kuendeleza Uislamu Nchini. Pia Mufti aliishukuru TIF kwa kumpatia zawadi ya Misahafu 5,000 na Juzuu Amma 20,000 kwa ajili ya kugawa visiwani humo. Katikati ni Katibu wa Mufti, Sheikh Fadhil Soraga.

NA MWANDISHI WETU

Taasisi ya The Islamic Foundation(TIF) inatarajia kumleta nchini mhadhiri wa kimataifa kutoka nchini Australia, Ustadh Wahaji Tarin ikiwa ni muendelezo wa juhudi za taasisi hiyo za zoezi kuwaleta wanazuoni wakubwa ulimwengu nchini kwa ajili ya da’wah. Mwaka jana TIF ilimleta nchini Mufti wa Zimbabwe na Mhubiri wa Kimataifa, Ismail bin Musa Menk. Mhadhiri anayekuja safari hii, Ustadh Tarin ni Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Australia na anatarajiwa kufanya mihadhara hapa nchini mwezi Aprili mwaka huu ambapo Aprili 16 atakuwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana. Na mihadhara itakayofuata itafanyika Aprili 17 mjini Morogoro katika ukumbi wa studio za Imaan saa mbili usiku hadi saa tatu, na kisha Aprili 20 atafanya mhadhara visiwani Zanzibar katika Chuo Kikuu cha Sumait kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana. Ustadh Tarin ni msomi wa mambo ya Sayansi katika fani ya ‘Extractive metallurgy’ na ana shahada ya pili katika masuala ya utawala katika biashara. Taarifa iliyotolewa na TIF yenye makao yake makuu mjini Morogoro inasema kuwa usajili kwa ajili ya watu watakaopenda kuhudhuria mihadhara hiyo utaanza kufanyika hivi ambapo watu watatangaziwa.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*