Updates

TIF yakabidhi misaada ya awamu ya pili Pemba

Taasisi ya The Islamic Foundation (TIF) yenye makao yake makuu mjini Morogoro imekabidhi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) awamu ya pili ya misaada ya zaidi ya tani 9 za vyakula mbalimbalikwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Pemba. Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa TIF, Mussa Buluki, ameliambia Gazeti Imaan kuwa misaada hiyo imetokana na Shilingi Milioni 28 ikiwa ni sehemu ya fedha Shilingi Milioni 112 zilizochangwa na wahisani mbalimbali wa ndani na nje kupitia kampeni ili- yoendeshwa na vyombo vya habari vya Radio na Tele- visheni za Imaan. “Kama ambavyo tuliahidi mara ya kwanza tumewe- za kuwasilisha jumla ya tani 22.5 za vyakula kwa ndu- gu zetu wa Pemba, pia katika awamu hii ya pili tume- leta tena misaada ya chakula takribani tani 9 ili kuwa- punguzia makali ya maisha ndugu zetu hawa,” alisema Buluki. Kwa mujibu wa Buluki, misaada hiyo itasambazwa kwa kaya 200 za Wilaya za Chake Chake na Mkoani am- bapo kila kaya (familia) itagawiwa jumla ya kilo 20 za mchele, kilo 10 za maharage, kilo 5 za sukari, kilo 5 za nga- no pamoja na mafuta ya kupikia lita 5. Katika maafa hayo iliripotiwa kuwa, zaidi ya nyumba 987 ziliezuliwa paa na nyingine zilibomoka kabisa ambapo kati ya hizo 447 zipo wilaya ya Chake Chake na 540 wilaya ya mkoani. Mbali na kuharibu nyumba, pia mvua hizo ziliharibu madaraja, misikiti na miundombinu ya maji na barabara. Katika kufanikisha zoezi hilo, vituo vya Radio na Tele- visheni za Imaan viliendesha vipindi maalum kwa ajili ya kuhamasisha watu kuchangia, ambapo watu wengi waliiti- kia wito huo kwa kutuma kwa kutuma michango yao kwa njia za simu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*