Updates

TIF yapokea tende kutoka Falme za Kiarabu

TAASISI ya The Islamic Founda- tion (TIF) imepokea kutoka katika Umoja wa Falme za Ki- arabu (UAE) zaidi ya boksi za tende kwa ajili ya kuzigawa katika maeneo

mbalimbali katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza baada ya tende hizo kuwasili nchini, Mwenyekiti wa TIF, Aref Nahdi ameushukuru Ubalozi wa Falme za Kiarabu nchi- ni kwa kusaidia Waislamu pamoja na Watanzania kwa ujumla katika

sekta mbalimbali. “Msaada huu wa tende ni moja tu kati ya misaada mingi ambayo Falme za Kiarabu imekuwa ikitoa kwa Watanzania na hivyo kusaidia maendeleo ya jamii,” Nahdi alisema.

Akizungumzia kuhusu tende hizo, Nahdi alisema kuwa zitasam-

bazwa katika taasisi mbalimbali kama vile BAKWATA, Dhinureyn na Ansary Muslim ili ziwe kugawi- wa kwa Waislamu bure. Aidha, Nahdi alisema tende nyingine zi- takabidhiwa kwa wakurungezi wa TIF katika mikoa mbalimbali ili wazigawe kwa walengwa.

Hata hivyo, Mwenyekiti Nahdi aliitaka jamii kutoa taarifa pindi watakapona tende hizo zinauzwa kwani kufanya hivyo ni kinyume na lengo la msaada huo. Alisema tende hizo ni bure hivyo atakayebainika kuuza hatua za kisheria zitachuku- liwe dhini yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*